IQNA

Serikali ya Austria kuzindia mpango wa kujasusi Waislamu

23:05 - July 21, 2020
Habari ID: 3472985
TEHRAN (IQNA) - Serikali ya Austria inatayarisha mpango wenye utata wa kuwaweka Waislamu wan chi hiyo chini ya uchunguzi mkali kwa lengo la kukabiliana na kile wanachodai ni ‘Uislamu wa Kisiasa.’

Chama cha mrengo wa kulia cha OVP kinasema mpango huo unalenga kuzuia  ‘chuki dhidi ya Mayahudi’ na misimamo mikali ya kidini.

Mpango huo umekosolewa vikali na wasomi pamoja na mashirika ya kutetea haki za binadamu.

Sera mpya dhidi ya Waislamu Austria ilitangazwa Januari Mosi na serikali ya mseto, ya chama cha mrengo wa kulia kinachojulikana kama Chama cha Watu wa Austria (OVP) na Chama cha Kijani, inaonekana kufuata sera za kibaguzi zilizokuwa zikifuatwa na serikali iliyotangulia.

Mwezi Mei mwaka jana, uchaguzi wa mapema uliitishwa Austria baada ya tuhuma za ufisadi dhidi ya chama cha mrengo wa kulia cha Uhuri wa Austria (FPO) na kiongozi wake wa zamani Heinz Christian Strache. Waustria, hasa raia wa kigeni waishio nchini humo walikaribisha kuunda serikali hiyo ya mrengo wa kulia.

Mamlaka ya Kiislamu Austraia (IGGO) ambayo inawakilisha Waislamu takribani 800,000 nchini Austria imeilaumu serikali mpya wa kuwa na sera zinazohasimiana na Waislamu. Aidha IGGO imesema imekatishwa moyo na Chama cha Kijani ambacho kinaonekana kuunga mkono sera hizo mpya zilizo dhidi ya Uislamu.

3472047

captcha