IQNA

Qiraa ya Qur’ani Tukufu ya Sheikh Mahmud Ali Al Banna + Video

23:17 - July 21, 2020
Habari ID: 3472986
TEHRAN (IQNA) – Mahmud Ali Al Banna alikuwa qarii mashuhuri wa Qur’ani aliyezaliwa katika kijiji cha Shobrabas kaskazini mwa Misri mnamo Disemba 17, 1926.

Mahmud Ali Al Banna alihifadhi Qur’ani kikamilifu akiwa na umri wa miaka 11 chini ya usimamizi wa Sheikh Moussa Al Muntash.

Baada ya kupata masomo ya kidini katika mji wa Tanta chini ya Sheikh Ibrahim Ibn Salam Al Maliki, alielekea Cairo mwaka 1945 na akaanza kupata umashuhuri kutokana na qiraa yake ya Qur’ani. Alitembelea maeneo mbali mbali duniani kusoma Qur’ani na hatimaye aliaga dunia Julai 20, 1985 sawa na 3 Dhul Qaada, 1405 Hijria Qamaria.

Hapa chini ni qiraa ya qarii huyo mashuhuri.

3911752

captcha