IQNA

Qiraa nadra ya Surat Al-Qadr ya Sheikh Abdul Basit

15:45 - August 10, 2020
Habari ID: 3473054
TEHRAN (IQNA) Klipu ya zamani na nadra ya Sheikh Abdul Abasit Abdulswamad akisoma Surat Al-Qadr imesambaa katika mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, qiraa hii ni ya miaka mingi iliyopita na ni yenye mvuto mkubwa  kwa kila anayesikiliza.

Abdul Basit alizaliwa mwaka 1927 katika kijiji cha Almazaizah katika eneo la Armant kusini mwa Misri. Sheikh Abdul Basit Abdul Swamad alikamilisha hifdhi ya Qur'ani akiwa na umri wa miaka 10 kijijini kwake kwa Ustadh Al Amir na akahitimu aina zote za kiraa ya Qur'ani akiwa na umri wa miaka 14.

Abdul Basit alipewa lakabu ya 'Koo ya Dhahabu' kutokana na kiraa yake ya kuvutia na alipendwa mno na wafuatiliaji wa masuala ya Qur'ani kwa kadiri kwamba hadi sasa anatambuliwa kuwa qarii mashuhuri na anayepesndwa zaidi wa Qur'ani.

Qari huyo mashuhuri wa Misri aliaga dunia tarehe 30 Novemba mwaka 1988 katika mji mkuu wa Misri, Cairo.

/3915831

Kishikizo: qiraa Abdulbasit misri
captcha