IQNA

Magaidi wakufurishaji waua watu 16 katika hujuma Mogadishu, Somalia

19:53 - August 17, 2020
Habari ID: 3473076
TEHRAN (IQNA) - Watu wasiopungua 16 wameuawa mjini Mogadishu Somalia na makumi ya wengine kujeruhiwa, kufuatia shambulio la magaidi wakufurishaji wa al-Shabab katika Hoteli ya Elite.

Vikosi maalumu vya Somalia vimetangaza kuwa, vimefanikiwa kumaliza uvamizi uliofanywa Jumalili katika hoteli iliyopo katika mji mkuu Mogadishu ambayo ilivamiwa na wananamgambo wa al-Shabab katika hoteli ya - Elite Hotel iliyopo katika eneo la ufukwe wa Lido, pamoja na wanamgambo kadhaa ambao idadi yao haijajulikana.

Watu wasiopungua 16 wameuawa mjini Mogadishu Somalia na makumi ya wengine kujeruhiwa, kufuatia shambulio la wanamgambo wa al-Shabab katika Hoteli ya Elite.

Vikosi maalumu vya Somalia vimetangaza kuwa, vimefanikiwa kumaliza uvamizi uliofanywa katika hoteli iliyopo katika mji mkuu Mogadishu ambayo ilivamiwa na wananamgambo wa al-Shabab katika hoteli ya - Elite Hotel iliyopo katika eneo la ufukwe wa Lido, pamoja na wanamgambo kadhaa ambao idadi yao haijajulikana.

Vikosi vya usalama viliizingira hoteli hiyo na kukabiliana kwa risasi na washambuliaji waliokuwa na silaha ndani ya hoteli. Saa nne baadae, msemaji wa serikali Ismael Mukhtar Omar alituma ujumbe kwenye ukurasa wa Twitter  akisema kuwa uvamizi huo umekwisha na wavamizi wote wameuawa.

Kwingineko, Jeshi la Somalia limewaua magaidi watano wa kundi la Al-Shabaab kwenye mapigano yaliyotokea katika kijiji cha Gof Gadud Burey kwenye mkoa wa kusini wa nchi hiyo.

Gavana wa eneo la Gof Gadud Burey Bw. Isak Ali Isak amewaambia wanahabari kuwa wapiganaji wa kundi la Al-shabaab walianza kushambulia kwa mabomu kambi ya jeshi la serikali kwenye eneo hilo Jumapili, lakini jeshi lilipambana nao, na kufanikiwa kuwaua watano kati yao.

Miongoni mwa watu waliouawa ni pamoja na afisa wa ngazi ya juu kutoka wizara ya habari na afisa mwingine kutoka wizara ya ulinzi nchini humo. Waziri wa Elimu wa Somalia amenusurika kifo katika shambulio hilo.

3472314/

captcha