IQNA

Hamas yaulani utawala wa Israel kwa kumkamata Sheikh Raed Salah

19:58 - August 17, 2020
Habari ID: 3473077
TEHRAN (IQNA) - Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imesema kuwa hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kumtia tena mbaroni kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Palestina ina lengo la kuwafutilia mbali walinzi wa Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem).

Msemaji wa Hamas, Hazim Qassim ameongeza kuwa mienedo ya kutumia mabavu ya Wazayuni dhidi ya Msikiti wa Al Aqsa na walinzi wa msikiti huo inadhiihrisha namna utawala wa Kizayuni unavyopuuza hisia za Waislamu duniani. 

Sheikh Raed Salah ambaye ni kiongozi wa Harakati ya Kiislamu katika ardhi ya Palestina iliyokaliwa kwa mabavu mwaka 1948 tangu jana asubuhi alipelekwa katika jela iliyo karibu na mji wa Haifa ili kutumikia kifungo chake. 

Mahakama ya utawala wa Kizayuni wa Israel imemhukumu kifungo cha miezi 28 jela kiongozi huyo wa Harakati ya Kiislamu ya Palestina kwa tuhuma eti za kuchochea ghasia na kuongoza harakati hiyo ya Kiislamu. 

Hivi karibuni Sheikh Salah ambaye ni mwenyekiti wa Harakati ya Kiislamu katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu yaani Israel, alishiriki katika warsha iliyoandliwa na Kamisheni ya Quds Tukufu ya Jukwalii la Kiraia la Ankara (ACSP) la Uturuki kabla ya kuanza kutumikia kifungo cha miezi 28 gerezani kuanzia Agosti 16.

Katika kikao hicho, alitahadharisha kuhusu njama za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Msikiti wa Al Aqsa ulio katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo.

3472319

captcha