IQNA

Jarida La Kifaransa lavunjia heshima Matukufu ya Kiislamu

12:54 - September 02, 2020
Habari ID: 3473129
TEHRAN (IQNA) - Kwa mara nyingine tena jarida hilo la Kifaransa la Charlie Hebdo limeamua kwa makusudi kuwafanyia kejeli na istihzai Waislamu na dini tukufu ya Uislamu kwa kuchapisha vibonzo vyenye kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu.

Vibonzo hivyo vimechapishwa wakati  leo Jumatano, ni siku ya kuanza kwa kesi dhidi ya watuhumiwa wa shambulizi dhidi ya makao makuu ya jarida hilo Januari 7 mwaka 2015.

Hii si mara ya kwanza kwa jarida hilo linalochapishwa nchini Ufaransa kukanyaga thamani za kidini pamoja na uhuru wa imani na itikadi za watu wengine, kwa kuwatusi Waislamu na matukufu yao.

Jarida la Charlie Hebdo limeshapicha mara kadhaa katuni na vibonzo dhidi ya dini hususan dhidi ya dini tukufu ya Uislamu na Mtume wake Muhammad SAW kwa kisingizio cha uhuru wa kujieleza, licha ya kukabiliwa na malalamiko makubwa ya Waislamu nchini Ufaransa na katika pembe mbalimbali za dunia. 

Haya yanajiri siku kadhaa baada ya watu wenye misimamo mikali ya kibaguzi kuuvunjia heshima Uislamu katika nchi za Norway na Sweden.

3920484/

captcha