IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Kiongozi Muadhamu alaani kitendo cha kuvunjiwa heshima Mtume SAW

19:31 - September 08, 2020
Habari ID: 3473148
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amelaani vikali hatua ya jarida la Ufaransa la Charlie Hebdo ya kuchapisha tena vibonzo vinavyomvunjia heshima Mtume Muhammad SAW na kusisitiza kuwa: Njama hizo za Marekani na utawala wa Kizayuni ni dhambi isiyosameheka.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo Jumanne na kuongeza kuwa, "dhambi kubwa na isiyosameheka ya jarida la Ufaransa ya kumtusi Mtume Mtukufu wa Uislamu Muhammad (saw) kwa mara nyingine tena, imedhihirisha chuki na uadui wa taasisi za kisiasa na kitamaduni za ulimwengu wa Magharibi dhidi ya Uislamu na Umma wa Kiislamu."

Amesema kisingizio cha 'uhuru wa kujieleza' kinachotumiwa na wanasiasa wa Ufaransa ili wasilaani jinai hiyo ni kosa kubwa na upotoshaji wenye maslahi ya kisiasa.

Ayatullah Khamenei ameeleza bayana kuwa: Sera za Wazayuni na madola ya kiistikbari zilizo dhidi ya Uislamu ndilo chimbuko la vitendo hivi vya kiuhasama.

Amebainisha kuwa, hatua hiyo ya jarida la Charlie Hebdo ya kuyavunjia heshima Matukufu ya Uislamu katika kipindi hiki, ni mpango wa serikali za Magharibi wa kujaribu kuyapotosha mataifa ya ulimwengu ili yasishghulishwe na njama za Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya eneo la Asia Magharibi.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa mwito kwa mataifa ya Kiislamu hususan katika eneo la magharibi mwa Asia kuwa macho juu ya masuala yanayohusu eneo hili hasasi, na kamwe yasisahau uadui wa wanasiasa na viongozi wa Magharibi dhidi ya Uislamu na Waislamu.

 

3472501

captcha