IQNA

Chuo Kikuu cha Qurani Sudan kuanza tena shughuli zake

21:03 - September 08, 2020
Habari ID: 3473150
TEHRAN (IQNA) – Shughuli za kielimu katika Chuo Kikuu cha Qur’ani nchini Sudan zimepangwa kuanza baada ya wiki chache.

Uamuzi huo umechukuliwa katika mkutano wa viongozi wa ngazi za juu wa chuo hicho.

Kwa mujibu wa taarifa,  wanafunzi wataanza masomo ya mwaka mpya wa kimasomo mnamo Oktoba 18.

Mkutano huo pia umejadili masuala ya wanafunzi, mipango ya chuo kikuu na changamoto zilizopo.

Kati ya mada muhimu iliyojadiliwa ni kuwekeza katika miundo msingi ya huduma za kusoma kwa njia ya intaneti.

Serikali ya Sudan imetnagaza kuanza kufungua vituo vya elimu nchini humo baada ya kufungwa kwa miezi kadhaa kutokana na janga la corona.

Hadi sasa watu 13,437 wameambukiza corona nchini Sudan huku wengine 833 wakipoteza maisha.

 

3921712

Kishikizo: sudan qurani tukufu
captcha