IQNA

Mashauriano kuhusu kufanyika mashindano ya kimataifa ya Qur’ani ya Iran kupitia intaneti

12:42 - September 09, 2020
Habari ID: 3473151
TEHRAN (IQNA) – Mashauriano yanaendelea kuhusu uwezekano wa kufanyika mashindano yajayo ya kimataifa ya Qur’ani ya Iran kwa njia ya intaneti.

Abbas Salimi, mkuu wa idara ya habari katika mashindano hayo amesema bado hakuna uamuzi wowote uliochukuliwa kuhusu kadhia hiyo.

Mwezzi Juni, Mehdi Qarasheikhlu, mkuu wa Idara ya Masuala ya Qur’ani katika Shirika la Wakfu la Iran alisema yamkini mashindano ya mwaka huu yasifanyike.

Mashindano ya 37 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Iran yalikuwa yafanyike mwezi Aprili lakini yaliakhirishwa kutokana na kuenea ugonjwa wa COVID-19.

Shirika la Wakfu la Iran huandaa mashindano hayo kila mwaka ambapo washiriki kutoka kona zote za dunia hualikwa.

Katika mashindano yaliyopita ya mwaka 2019, kulikuwa na washiriki kutoka nchi 80 ambao walishindana katika kuhifadhi na kusoma Qur’ani Tukufu.

Ripoti mpya zinaonyesha kuwa, watu wasiopungua 27,312,733 wameambukizwa virusi vya corona duniani kote hadi sasa, ambapo 893,463 miongoni mwao wamefariki dunia.

3921844

captcha