IQNA

Rais Hassan Rouhani

Marekani haiwezi kuvunja mapambano ya taifa la Iran kwa kuzuia dawa na chakula

17:13 - October 09, 2020
Habari ID: 3473244
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Marekani haitaweza kuvunja mapambano na muqawama wa taifa la Iran kwa kuweka vizingiti vya kununua na kudhamini dawa na chakula.

Rais Hassan Rouhani ameyasema hayo leo katika mazungumzo yake na Gavana wa Benki Kuu ya Iran akizungumzua njama zinazofanywa na serikali ya Marekani dhidi ya Iran na kuongeza kuwa, hatua zinazochukuliwa na serikali ya Marekani katika fremu ya jitihada za kipropaganda na kisiasa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu zina malengo ya ndani ya Marekani kwenyewe. 

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema hatua zinazochukuliwa hivi sasa na serikali ya Washington ni mwendelezo wa makosa ya kistratijia ya Donald Trump ya kujiondoa katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA. Ameongeza kuwa, kwa kutegemea uchambuzi usio sahihi, serikali ya Marekani iliamini kwamba, vikwazo hivyo vitavunja mapambano na kusimama kidete kwa taifa la Iran na kuliweka taifa katika matatizo; lakini tajiriba imeonyesha kuwa uchambuzi huo haukuwa sahihi hata kidogo na wala haufai.

Rais Rouhani amesema Marekani imekuwa ikishindwa na kufeli mara zote kutokana na kukariri makosa ya kistratijia, na mfano wake wa karibuni ni kutaka kuhuisha utaratibu wa "Snapback Mechanism" wa kurejesha vikwazo vya silaha dhidi ya Iran katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Amesema nchi zote zinaona kwamba hatua hizo za Marekani ni kinyume cha sheria na kanuni za kimataifa, na katika kipindi hiki cha maambukizio ya virusi vya corona, hatua hizo za Marekani zinahesabiwa kuwa ni dhidi ya binadamu.

Amesisitiza kuwa nchi zinazodai kutetea haki za binadamu duniani zinapaswa kulaani hatua hizo za Marekani.

3928219

captcha