IQNA

Al Azhar yataka usawa katika usambazwaji chanjo ya corona

21:59 - November 17, 2020
Habari ID: 3473367
TEHRAN (IQNA) – Sheikh Ahmed el-Tayeb, mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha al Azhar ametoa wtio wa kusambazwa chanjo ya corona au COVID-19 kwa usawa.

Katika ujumbe kupitia ukurasa wake wa Facebook, Sheikh el-Tayeb amepongeza jitihada za wanasayansi walio mbioni kutengeneza chanjo ya corona duniani.

Amewataja wanasayansi hao kuwa mashujaa ambao watapata baraka za Mwenyezi Mungu kutokana na jitihada zao za  kukabiliana na changa la corona ambalo hadi sasa limeangamiza watu zaidi ya milioni moja duniani huku mamilioni ya wengine wakiwa wanakabiliwa na hatari.

El-Tayeb ameongeza kuwa chanjo ya corona ikipatikana, inapaswa kusambazwa kwa uadilifu.

Amesema watu w asiojiweza katika jamii wakiwemo wakimbizi hawapasi kusahauliwa katika usambazwaji wa chanjo.

Siku ya Jumatatu, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilibainisha matumaini yake kuwa chanjo ya corona itapatikana duniani kuanzi kati kati ya mwaka ujao. Walioambukizwa corona duniani hadi sasa ni milioni 55 na waliofariki ni zaidi ya milioni 1.3.

3935805

 

 

Kishikizo: Corona chanjo al azhar
captcha