IQNA

Raia wa Chad ateuliwa kuwa Katibu Mkuu wa OIC

16:25 - November 29, 2020
Habari ID: 3473404
TEHRAN (IQNA) - Mwanadiplomasia Hussein Ibrahim Taha, aliyewahi kuwa Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Chad ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC akichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa Msaudia Yousef bin Ahmad Al-Othaimeen.

Hussein Ibrahim Taha atachukua rasmi wadhifa huo Novemba mwakani yaani mwaka mmoja ujao wakati Yusuf al-Uthaimeen atakapomaliza muda wake.

Uteuzi huo umefanyika katika mkutano wa siku mbili wa 47 wa Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC uliokuwa ukifanyika huko Niamey mji mkuu wa Niger.

Kikao cha 47 cha Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kilifanyika tarehe 27 za 28 mwezi huu huko Niamey mji mkuu wa Niger.

Kikao hicho kimefanyika huku usaliti uliofanywa na baadhi ya nchi za Kiarabu katika eneo la Mashariki ya Kati kwa Palestina kwa hatua yao ya kuanzisha uhusiano rasmi na utawala ghasibu wa Kizayuni unaoikalia Quds kwa mabavu ukiwakasirisha wananchi na baadhi ya wakuu wa nchi za Kiislamu duniani. 

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imekuwa ikikosolewa kutokana na kutokuwa na misimamo imara kuhusiana na masuala mbalimbali ya Waislamu ikiwemo kadhia ya Palestina huku baadhi ya wanachama wake kama wakiungana na adui Mzayuni baada ya kutangaza rasmi kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.

3473256

Kishikizo: oic CHAD IBRAHIM TAHA
captcha