IQNA

Shahidi Fakhrizadeh azikwa Tehran, Iran yasema itajibu jinai

19:59 - November 30, 2020
Habari ID: 3473407
TEHRAN (IQNA)- Shughuli ya maziko ya mwili wa shahid Mohsen Fakhrizadeh, mwanasayansi mkubwa wa nyuklia na masuala ya kijeshi wa Iran imefanyika leo Jumatatu kwa kuchungwa protokali zote za kiafya ili kujiepusha na maambukizi ya corona.

Shughuli hizo zimefanyika katika Wizara ya Ulinzi hapa Tehran na kuhudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu wa kiserikali na kijeshi wa Iran. Shahid Fakhrizadeh amezikwa katika haram ya Imamzadeh Saleh hapa mjini Tehran.
Wakati huo huo, Waziri wa Ulinzi wa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, hakuna jinai, mauaji na kitendo chochote cha kijinga litakakachofanyiwa taifa la Iran ambacho kitaachwa bila kujibiwa.

Brigedia Jenerali Amir Hatami ameyasema hayo katika shughuli ya mazishi ya shahid Shahidi Fakhrizadeh, mwanasayansi bora wa nyuklia na ulinzi wa Iran na akasisitiza kwamba: watenda jinai wajue kwamba itawafika adhabu tu kwa walichokifanya.

Brigedia Jenerali Hatami ameyashukuru mataifa na nchi zilizoonyesha kuchukizwa na jinai ya mauaji ya kigaidi ya mwanasayansi wa nyuklia wa Iran na akazionya nchi na tasisi za kimataifa zilizoipuuza jinai hiyo kwamba, kuwaunga mkono magaidi ambao ni washenzi na mafidhuli kunazidisha ushenzi na ufidhuli wao; na ugaidi huo utawaandama na kuwalenga wao pia katika siku za usoni.

Magaidi wenye silaha siku ya Ijumaa ya tarehe 27 Novemba waliishambulia gari iliyokuwa imembeba Mohsen Fakhrizadeh, Mkuu wa Shirika la Utafiti na Ubunifu la Wizara ya Ulinzi ya Iran na kumuua shahidi mwanasayansi huyo mkubwa wa nyuklia na masuala ya ulinzi. Nchi nyingi duniani ikiwemo Russia, China, Venezuela, Afrika Kusini na Uturuki zimelaani mauaji hayo ya kigaidi ya shahid Mohsen Fakhrizadeh.

3938244

 

captcha