Kauli hiyo ya afisa huyo wa afya Malaysia inaondoa wasiwasi uliopi miongoni mwa Waislamu kuwa yamkini chanjo ya COVID-19 ina mada ambazo zimeharamishwa katika Uislamu.
Alhamisi iliyopita, Baraza la Kitaifa la Masuala ya Kiislamu lilikutana kujadili iwapo Waislamu wanaweza kupata chanjo ya COVID-19. Waziri wa Masuala ya Kidini Malaysia, Zulkifli Mohammad Al Bakri alisema uamuzi wa mwisho utatangazwa baada ya kuwasilishw akwa mfalme, ambaye husimamia masuala ya kidini nchini humo.
Shirika la dawa la Malaysia, Pharmaniaga, linapanga kujenga kiwanda cha kwanza cha chanjo halali mwaka 2022. Malaysia tayari imeshatia saini mikataba na mashirika ya COVAX na Pfizer kwa ajili ya kupata chanjo ya COVID-19 kwa ajili ya asilimia 20 ya wale ambao ni dharura kupata chanjo.