IQNA

Marekani yakiwekea vikwazo Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa SAW

23:43 - December 09, 2020
Habari ID: 3473440
TEHRAN (IQNA)- Katika muendelezeo wa vikwazo vya kidhalimu vya Marekani dhidi ya Iran, Wizara ya Fedha ya nchi hiyo imetangaza vikwazo dhidi ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa SAW na balozi wa Iran nchini Yemen Hassan Irloo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, vikwazo dhidi ya chuo kikuu hicho na mwanadipolomasia huyo vimetangazwa katika amri iliyotolewa Jumanne na serikali ya Marekani.

Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa SAW ni chuo Kiislamu ambacho kilianzishwa kwa lengo la kueneza mafunzo ya Kiislamu kupitia teknolojia na mbinu za kisasa.

Chuo hicho huwapa fursa wanafunzi kutoka kone zote za dunia kupata elimu na kujifunza sayansi za Kiislamu.

Kwa mujibu wa amri hiyo ya Jumanne ya Wizara ya Fedha ya Marekani mali zote ambazo zinamilikiwa na chuo hicho na zile ambazoo umiliki wa zaidi ya asilimia 50 ni wa chuo hicho, na ambazo ziko katika mamlaka ya Marekani, zitawekewa vikwazo. Aidha raia wa Marekani kwa ujumla wanazuia kuamiliana na chuo hicho.

Halikadhalika benki za kigeni ambazo zitashiriki katika miamala ya kifedha na chuo hicho zinaweza kuwekewa vikwazo na kuzuiwa kutumia mfumo wa kifedha wa Marekani.

Kuhusiana na balozi wa Marekani nchini Yemen, Marekani imedai anahusika katika kuipa nguvu harakati ya Ansarullah.

Vikwazo hivyo ni katika sera za Marekani za ‘mashinikizo ya juu zaidi dhidi ya Iran’. Wakuu wa Washington wamemaliza orodha yote ya vikwazo ambavyo walikuwa wamekusudia kuiwekea Iran na kwa msingio huo wameanza sasa kulenga vikuu ambavyo vinawasiadia vijana wengi kupata elimu na kujiendeleza kimaisha kwa maslahi ya nchi zao.

Hivi karibuni Televisheni ya Bloomberg ilisema sera za Marekani za  vikwazo dhidi ya Iran zimegonga mwamba na kwamba watawala wa Washington wameishiwa na machaguo zaidi ya kuiwekea Iran vikwazo.

3939936

captcha