IQNA

Ensaiklopedia ya miujiza ya kisayansi katika Qur'ani yachapishwa Algeria

11:42 - December 11, 2020
Habari ID: 3473445
TEHRAN (IQNA) –Ensaiklopedia ya miujiza ya sayansi katika Qur'ani Tukufu imechapishwa hivi karibuni nchini Algeria.

Tovuti ya echoroukonline imeandika kuwa ensaiklopedia hiyo ambaye imeandikwa na Heithan Joma Hilal imechapishwa na Taasisi ya Dar al-Izzah wa al-Kiramah.

Mwandishi wa ensaiklopedia hiyo amejikita katika nukta za kisayansi za muujiza wa Qur'ani Tukufu ambapo anaashiria aya za Qur'ani kuhusu maumbile ya mwanadamu, mbingu na ardhi.

Katika  dibaji ya ensaiklopedia hiyo, ameandika kuwa Qur'ani Tukufu inahimiza kuhusu ulazima wa kutafakari kuhusu aya za Kitabu hicho.

Ustawi wa sayansi umeweza kubainisha wazi baadhi ya miujiza ya Qur'ani Tukufu na jambo hilo linaweza kutumika katika kuwajulisha walimwengu nuru ya Qur'ani.

Kuna aya nyingi za Qur'ani kuhusu masuala ya kimaumbile kama vile kuumbwa bingu, maji, chimbuko la dunia, kiinitete cha mwanaadamu n.k.

Wale waliofanya utafiti kuhusu miujiza ya Qur'ani wanasema Kitabu hicho kitakatifu kimeashiria masuala kama hayo mara katika idadi kubwa ya aya.

Katika karne iliyopita wanazuoni wa Qur'ani wamekuwa wakifanya utafiti kuhusu miujiza ya kisayansi katika Qur'ani tukufu. Miongoni mwa wanazuoni hao ni Muhammad b. Ahmad al-Iskandarani, Rashid Rida, na Tantawi.

3473354

captcha