IQNA

Qarii ya Sheikh Taruti akisoma aya za Sura za Al-Ahzab, At-Takwir (+Video)

18:19 - December 23, 2020
Habari ID: 3473485
TEHRAN (IQNA) Hivi karibuni Televisheni ya Qur’ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilirusha hewani qiraa ya Qur’ani Tukufu ya Sheikh Abdul Fattah Taruti wa Misri.

Qiraa ya qarii huyo mashuhuri wa Misri ilikuwa ya aya  kadhaa za Surah Al-Ahzab na Surah At-Takwir za Qurani Tukufu.

Sheikh Taruti alizwaliwa mwaka 1965 katika kijiji cha Tarut karibu na mji wa Zagazig jimboni Sharqia. Alianza kuhifadhi Qur’ani akiwa na umri wa miaka mitatu na alifanikiwa kuhifadhi Qur’ani kikamilifu akiwa na umri wa miaka 8. Taruti alisoma katika tawi la Zagazig la Chuo Kikuu cha Al Azhar na aliendelea  kuimarisha uwezo wake wa Qur’ani kwa kupata mafunzo kwa kutoka kwa wasomi wakubwa kama vile Sheikh Mohammad Al-Lithi, Shahat Anwar na Saeed Abdul Samad.

3942387

captcha