IQNA

Kiongozi Muadhamu awatakia kheri Wakristo katika siku kuu ya Krismasi

13:18 - December 26, 2020
Habari ID: 3473492
TEHRAN (IQNA) -Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewatumia ujumbe Wakristo wa Iran na duniani kwa ujumla akiwatakia kheri wakati wakisherehekea Krismasi.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema katika ujumbe wake kupitia Twitter na ambao ameutuma kwa lugha ya Kiingereza kwamba, anawatakia kheri Wakristo wa Iran na duniani kiujumla katika sherehe za za Krismasi za kukumbuka kuzaliwa Nabii Isa mwana wa Maryam AS.

Katika ujumbe huo, Ayatullah Khamenei amesema: "ninatoa mkono wa baraka kwa Wakristo na Waislamu kote duniani na hasa raia wenzangu wa Iran wa dini ya Kikristo kwa mnasaba wa maadhimisho ya siku ya kuzaliwa Nabii Isa Masih- Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe Juu Yake-."

Wakristo duniani, jana Ijumaa waliadhimisha sikukuu ya Karismasi wanayoinasibisha na siku ya kuzaliwa Nabii Isa mwana wa Maryam AS, sherehe ambazo hufanyika tarehe 25 Disemba kila mwaka. 

3473505

captcha