IQNA

Sayyid Hassan Nasrallah

Mauaji ya Shahidi Soleimani yalitekelezwa na pande tatu za Israel, Marekani na Saudi Arabia

18:39 - December 28, 2020
Habari ID: 3473500
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema, kusudio la kuwaua viongozi na makamanda wa harakati hiyo ya muqawama wa Kiislamu ni lengo la pamoja la Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel na akabainisha kwamba, zimetolewa indhari na masisitizo na duru tofauti kuhusu uwezekano wa yeye kuuawa katika kipindi cha karibuni.

Sayyid Hassan Nasrallah ameyasema hayo katika mahojiano maalumu na televisheni ya al-Mayadeen na akabainisha kuwa, kabla ya kuuliwa shahidi kamanda Qassem Soleimani na hata baada yake, yeye alikuwa miongoni mwa wale ambao Marekani na utawala wa Kizayuni zilipanga kuwaua; na hata kabla ya kufanyika uchaguzi wa rais wa Marekani zilifanywa juhudi kubwa zaidi kufanikisha lengo hilo kwa sababu Trump alihitaji kuchukua hatua kama hiyo kwa ajili ya kuathiri matokeo ya uchaguzi kwa manufaa yake.

Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema, hata utawala wa Saudi Arabia pia umedhamiria kumuua; na akaongeza kwamba, wakati mrithi wa ufalme wa Saudia Mohammad bin Salman alipokuwa safarini nchini Marekani aliitaka Washington imfanyie kazi hiyo.

Sayyid Hassan Nasrallah amesema, kinyume na mauaji ya shahid Imad Mughniya (mmoja wa makamanda wa Hizbullah ya Lebanon aliyeuliwa nchini Syria) na mauaji ya shahid Mohsen Fakhrizadeh (mwanasayansi wa nyuklia na masuala ya ulinzi wa Iran), mauaji ya makamanda shahid Qassem Soleimani na shahid Abu Mahdi al Muhandis yalifanywa hadharani; na mauaji hayo ni miongoni mwa njama na mpango wa pamoja wa pande tatu za Israel, Marekani na Saudi Arabia.

Amesisitiza kwamba: "Jinai ya kumuua kigaidi shahid kamanda Suleimani si jinai ya Marekani peke yake, bali Israel na Saudia pia zilihusika na zilishiriki katika jinai hiyo."

Katika mahojiano hayo maalum na televisheni ya al-Mayadeen, Katibu Mkuu wa Hizbullah ameeleza pia kwamba, Marekani iliamini kuwa kwa kumuua shahidi Qassem Soleimani na Abu Mahdi al-Muhandis, itaumaliza mhimili wa muqawama, ilhali mhimili huo haujafungamana na mtu mmoja au wawili na wala hautakuwa hivyo.

Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa rais aliyeko madarakani nchini Marekani kuchukua hatua ya kufanya kitu chochote kile katika siku zijazo, Sayyid Hassan Nasrallah amesema, upo uwezekano wa kutokea chochote kile hasa kutokana na shakhsia ya Trump ya upunguani na umajinuni mkubwa alionao, lakini kauli na hatua zote hizo zinachukuliwa katika muelekeo wa vita vya kisaikolojia vya Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya mhimili wa muqawama au mapambano ya Kiislamu.

3943772

captcha