IQNA

Wapalestina Ghaza wamkumbuka Shahidi Soleimani

21:20 - January 05, 2021
Habari ID: 3473528
TEHRAN (IQNA)- Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza wameandaa khitma kwa mnasaba wa kuwadia mwaka moja tokea auawe shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani.

Kwa mujibu wa taarifa, Khitma hiyo imehudhuriwa na wanachama wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) na Harakati ya Jihad Islamu.

Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, ambaye alikuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amekumbukwa katika kikao hicho kilicho fanyika chini ya anuani ya ‘Shahidi wa Quds’ kama mmoja kati ya waungaji mkono wakubwa wa harakati za ukombozi wa Palestina. Khitma

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) alielekea Iraq Januari 3 mwaka 2020 kufuatia mwaliko rasmi wa wakuu wa Iraq.

Punde baada ya kuwasili Iraq aliuawa shahidi katika hujuma ya ndege za kivita za jeshi vamizi na la kigaidi la Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad. Aidha katika hujuma hiyo ya kigaidi Abu Mahdi Al Muhandis, Naibu Mkuu wa Harakati ya Kujitolea ya Wananchi wa Iraq, naye pia aliuawa shahidi akiwa ameandamana na Qassem Soleimani. Watu wengine wanane waliokuwa katika msafara huo nao pia waliuawa shahidi.

Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani alikuwa na nafasi kubwa katika mapambano na maadui pamoja na magaidi na pia katika kuangamiza kundi la kigaidi la Daesh au ISIS. Pia alikuwa nguzo muhimu katika harakati za kupigania ukombozi wa Palestina. Halikadhalika alikuwa na nafasi muhimu katika kusambaratisha njama ya Marekani na Wazayuni ya kuligawa eneo vipande vipande.

3473608

captcha