IQNA

Ufaransa yafunga misikiti tisa, Waislamu wazidi kukandamizwa

15:14 - January 16, 2021
Habari ID: 3473563
TEHRAN (IQNA) – Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Gérald Darmanin ametangaza uamuzi wa kufunga misikiti tisa nchini humo katika kile kinachoonekana kuwa ni kukithiri ukandamizaji wa Waislamu nchini humo.

"Maeneo tisa kati ya 18 ambayo tulikuwa tunayachunguza yamefungwa kufuatia amri yangu," amesema  Gérald Darmanin  katika ujumbe kupitia Twitter."

"Tunachukua hatua kali dhidi ya watu wenye misimamo ya Kiislamu wanaotaka kujitenga," ameongeza.

Mnamo Pili Disemba 2020, Darmanin alitangaza oparesheni maalimu ya kuchunguza misikiti au kumbi za swala 76 kte Ufaransa.

Imedokezwa kuwa aghalabu ya misikiti iliyofungwa iko katika eneo la Parisian na sababu zimetajwa kuwa za kiusimamizi na kutozingatia masuala ya usalama. Mbali na misikiti pia kumbi za swala za Waislamu pia zimefungwa katika oparesheni hiyo.

Serikali ya Ufaransa hivi karibuni ilipendekeza sheria mpya ambayo inaonekana kuwalenga Waislamu ambao hawakubaliani na mfumo unaotawala nchini humo.

Sheria hiyo ambayo inajulikana kama 'Ustawshaji wa Heshima kwa Misingi ya Jamhuri' pia inajulikana kama sheria ya kupinga wanaotaja kujitenga inatazamiwa kufikishwa bungeni Februari 1.

Mapema leo Jumamosi, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa amekutana na wakuu wa Baraza la Uislamu Ufaransa kujadili kile ambacho serikali ya Paris inakitaja kuwa ni 'mradi wa kuleta mabadiliko katika Uislamu' nchini Ufaransa.

Katika mradi huo, serikali ya Ufaransa inataka kuhakikisha kuwa Uislamu unaendeleana na thamani za mfumo wa Jamhuri unaotawala nchini humo.

Sheria hiyo inakinzana moja kwa mja na mafundisho ya Kiislamu huki ikiunga mkono thamani za usekulari ambao  kimsingi  unaihesabu dini kuwa inaishia katika matendo ya mtu binafsi tu na kuzuia kuingia dini katika masuala ya kijamii na kisiasa.

3473713

captcha