IQNA

Washiriki kutoka nchi 70 katika nusu fainali mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran

8:16 - January 18, 2021
Habari ID: 3473568
TEHRAN (IQNA)- Nusu fainali ya Mashindano ya 37 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran inaanza Jumanne Januari 19.

Hayo yamedokezwa na Mehdi Qarasheikhlu, Mkuu wa Masuala ya Qur'ani katika Shirika la Wakfu na Misaada la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Katika mahojiano na IQNA, amesema semi fainali ya mashindano hayo itajumuisha washiriki 120 kutoka nchi 70. Washiriki takribani 50 wanatazamiwa kufika fainali ya mashindano hayo ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu.

Aidha amesema katika duru za awali kulikuwa na washiriki 600 kutoka nchi 70. Ameongeza kuwa, mashindano hayo ya semi fainali ambayo yanafanyika kwa njia ya intaneti yataendelea hadi Januari 21.

Shirika la Wakfu la Iran huandaa mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani kila mwaka.

Kutokana na janga la COVID-19 mashindano hayo hayakufanyika mwaka 2020 na yalifanyika mara ya mwish Aprili 2019 mjini Tehran ambapo kulikuwa na washiriki kutoka nchi zaidi ya 36.

3947912

captcha