IQNA

Qiraa ya Qur'ani ya El-Minshawi akiwa na sauti ya huzuni + Video

16:14 - January 20, 2021
Habari ID: 3473575
TEHRAN (IQNA) – Leo Januari 20 ni mwaka 101 wa kumbukumbu ya kuzaliwa mmoja kati ya wasomjai bingwa wa Qur'ani Tukufu nchini Misri.

Mohammad Siddiq El-Minshawi ni maarufu kwa sauti yake yenye mvuto.

El-Minshawi alizaliwa Januari 1920 katika mji wa Al Minshah katika jimbo la Sohag nchini Misri na alilelewa na kuinukia katika familia ya wasomaji Qur'ani. Alifanikiwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu akiwa na umri wa miaka 8 na mwaka mmoja baadaya akaanza kujifunza kusoma Qur'ani kitaalamu.

Baada ya muda usio mrefu Minshawi alipata umashuhuri kama qarii ambaye alikuwa akitumia mbinu za Tarteel na Tahqiq katika usomaji wake.

Alisafiri katika nchi nyingi duniani kwa ajili ya usomaji Qur'ani zikiwemo Indonesia, Jordan, Saudi Arabia, Syria, Iraq, Pakistan na Sudan.

Aliaga dunia mwaka 1969 akiwa na umri wa miaka 49.

Misri ni mashuhuri duniani kama nchi ambayo imeweza kutoa wasomaji bora zaidi wa Qur'ani Tukufu katika miongoi ya hivi karibuni.

3948722

Kishikizo: Minshawi qarii
captcha