IQNA

Mufti wa Quds alaani kiteno cha Israel kuzuia ukarabati wa Msikiti wa Al Aqsa

11:53 - January 28, 2021
Habari ID: 3473597
TEHRAN (IQNA) - Sheikh Mohammad Hussein, Mufti Mkuu wa Quds (Jerusalem) ameulaani vikali utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kuzuia ukarabati wa Msikiti wa Al Aqsa.

Sheikh Hussein na mamufti wengine wa Quds walikutana Jumatano na kulaani utawala ghasibu wa Israel kwa kuzuia ukarabati wa Al Aqsa na pia ukarabati wa Msikiti wa Ibrahimi katika mji wa Al Khalil (Hebron) kusini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Wanazuoni hao wa Kiislamu wametoa wito kwa taasisi za kimataifa, ikiwemo UNESCO, kuchukua hatua za kivitendo kukabiliana hatua za ukiukwaji sheria za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Utawala wa Kizayuni wa Israel umekalia kwa mabavu eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Quds Mashariki baada ya vita na za Kiarabu mwaka 1967. Aidha utawala wa Israel ulikalia Quds Mashariki, hatua ambayo haitambuliwi kimataifa.

3950287

captcha