IQNA

Umoja wa Mataifa walaani vikali hujuma kigaidi Mogadishu

17:25 - February 02, 2021
Habari ID: 3473615
TEHRAN (IQNA)- Umoja wa Mataifa umelaani vikali shambulizi la kigaidi lilofanywa Jumapili kwenye 'Hotel Afrika' katika mji mkuu Mogadishu na kusababisha vifo vya watu kadhaa na wengine wengi kusalia majeruhi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa taarifa kupitia msemaji wake Jumatatu ambapo amelaani vikali hujuma ya kigaidi dhidi ya 'Afrik Hotel' majini Mogadishu.

Watu tisa wanaripptiwa kupoteza maisha katika hujuma hiyo huku wengine 10 wakijeruhiwa.

Guterres ametuma salamu za rambi rambi kwa familia za waliouawa huku akisisitiza kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kuunga mkono serikali yakifederali ya Somalia katika jitihada zake za kurejesha amani nchini humo.

Aidha Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia James Swan ametoa taarifa na kusema kuwa wamechukizwa na shambulio hilo kwenye eneo hilo ambalo mara nyingi hutembelewa na raia.

Kwa mujibu wa ripoti, magaidi wakufurishaji wa Al Shabaab wamekiri kuhusika na shambulio hilo Jumapili mchana na kisha kushikilia kwa muda mrefu hoteli hiyo kabla ya kuzidiwa nguvu baadaye na vikosi vya usalama vya Somalia.

Vyombo vya habari vinaripoti kuwa raia kadhaa waliokuwa wamekwama ndani ya hoteli waliokolewa na vikosi hivyo vya usalama vya Somalia.

Swan ametuma salamu za rambirambi kwa familia za wafiwa huku akiwatakia ahueni ya haraka majeruhi.

Somalia iliyoko kwenye pembe ya Afrika, imekuwa ikikabiliwa na mashambulio ya mara kwa mara ya kigaidi ambapo kikundi cha Al Shabaab kimekuwa kikiri kuhusika nayo.

Katika shambulio kama hilo mwezi Agosti mwaka jana wa 2020, takribani watu 17 waliuawa baada ya magaidi hayo kushambulio hoteli ya Elite, tukio ambalo lilisababisha mapigano ya saa saba kati ya Al Shabaab na vikosi vya usalama vya Somalia.

Somalia ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1992 baada ya kuangushwa utawala wa Siad Barre. Katika miaka ya hivi hivi karibuni nchi hiyo imeshuhudia kushadidi hujuma za magaidi wa al-Shabab na hivyo kuwasababishia raia wa nchi hiyo matatizo makubwa.

Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika maarufu kama AMISOM wanaokadiriwa kufikia 21,000 wamekuweko nchini Somalia tokea mwaka 2007 ili kujaribu kukabiliana na magaidi wa al-Shabab. Hatahivyo pamoja na vitihada hizo za kimataifa, magaidi wa al-Shabab wanaendelea kutekeelza hujuma Somalia na nchi jirani ya Kenya.

3951481

captcha