IQNA

Uamuzi wa ICC dhidi ya Israel waungwa mkono na OIC, Al Azhar

20:58 - February 08, 2021
Habari ID: 3473631
TEHRAN (IQNA) – Uamuzi wa hivi karibuni wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) wa kuchunguza jinai za Israel dhidi ya Wapalestina umeungwa mkono na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) na chuo cha Kiislamu cha Al-Azhar nchini Misri.

Katika taarifa ICC imesema uamuzi huo ni ushindi wa sheria za kimataifa. Aidha Sheikh Mkuu wa Al Azhar Sheikh Ahmed el Tayyeb amepongeza uamuzi huo na kusema umewaletea matumaini Wapalestina kwamba wanaweza kupata haki walizopokonywa.

Aidha ametoa wito kwa jamii ya kimataifa hadi pale nchi huru ya Palestina intakapoundwa mji mkuu wake ukiwa ni Quds au Jerusalem.

Kufuatia ombi la Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina kwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC kwa ajili ya kuchunguza jinai za utawala wa kigaidi wa Israel dhidi ya taifa la Palestina, majaji wa mahakama hiyo wametoa uamuzi wakisema kuwa mahakama hiyo inafaa kisheria kuchunguza jinai za kivita katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo.

Hukumu hiyo imetolewa katika hali ambayo mwezi Disemba 2019, Fatou Bensouda, mwendesha mashtaka mkuu wa ICC alisema kuwa kulikuwepo na ushahidi wa kutosha uliothibitisha kwamba kuna jinai za kivita ambazo zilitekelezwa katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan yakiwemo maeneo ya Quds Mashariki na vile vile katika Ukanda wa Gaza. Kufuatia kutolewa tuhuma za jinai za kivita dhidi ya utawala ghasibu wa Israel, ombi lilitolewa kwa majaji wa Mahakama ya ICC kwanza wachunguze iwapo mahakama hiyo ilifaa kisheria kufanya uchunguzi kuhusu jinai hizo au la.

Hivi sasa mahakama hiyo imetia uamuzi ikithibitisha kuwa inayo ustakihi wa kisheria wa kuchunguza na kufuatilia jinai zilizotekelezwa na utawala haramu wa Israel katika ardhi unazozikalia kwa mabavu tokea mwaka 1967, yaani Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, unaojumuisha pia Quds Mashariki. Kwa mujibu wa maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, mipaka ya 1967 inahesabika kuwa mipaka ya ardhi za Palestina na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi hizo ni kinyume cha sheria, jambo ambalo limekuwa likikukwa wazi na utawala wa Kizayuni.

3952750

captcha