IQNA

Algeria yafungua misikiti yote baada ya maambukizi ya Corona kupungua

20:47 - February 16, 2021
Habari ID: 3473655
TEHRAN (IQNA)- Algeria imefungua misikiti yote nchini humo baada kwa ajili ya sala za jamaa za kila siku na Sala ya Ijumaa.

Ofisi ya Rais wa Algeria imesema maeneo yote ya ibada ya yatafunguliwa lakini kwa sharti la kuzingatia kanuni za kiafya za kuzuia maambukizi ya Corona au COVID-19.

Uamuzi huo umechukuliwa baada ya kupungua kesi za maambukizi ya corona nchini Algeria.

Pamoja na hayo, Ofisi ya Rais wa Algeria imesema sheria ya kutotoka nje usiku itaendelea kutekelezwa kuanzia saa nne usiku hadi saa 11 Alfajiri kwa muda wa wiki mbili zaidi katika mikoa 19 kati ya mikoa yote 48 nchini humo.

Hali kadhalika sherehe mbali mbali, mijimuiko ya kifamilia na maandamano ni marufuku nchini humo kwa ajili ya kuzuia kuenea Corona.

Algeria pia imeshazindua kampeni ya chanjo ya COVID-19 ambayo imeundwa nchini Russia ijulikanayo kama Sputnik V.

Hadi sasa watu zaidi ya 110,000 wameambukizwa Corona nchini Algeria na miongoni mwao zaidi ya 3,000 wamefariki.

3954286

Kishikizo: algeria Corona waislamu
captcha