IQNA

Katibu Mkuu wa UN alaani utekaji nyara wanafunzi nchini Nigeria

21:40 - February 28, 2021
Habari ID: 3473690
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amelaani utekaji nyara wa wanafunzi zaidi ya 300 katika jimbo la Zamfara kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Katika taarifa Guterres ametaka wanafunzo hao waachiliwe haraka na bila masharti ili warejee aktika familia zao. Amesema hujuma dhidi ya shule na vituo vya kieleimu ni ukiukwaji wa wazi wa haki za watoto na haki za binadamu.

Mashambulio ya kigaidi yangali yanaendelea katika nchi za magharibi mwa Afrika na hasa nchini Nigeria. Katika mashambulio ya karibuni kabisa, mamia ya wanafunzi wametekwa nyara nchini humo kufuatia shambulio lililofanywa na wabeba silaha katika shule moja katika jimbo la Zamfara, kaskazini mwagharibi mwa nchi hiyo.

Katika miezi kadhaa iliyopita, makundi hayo yameimarisha shughuli zao za kigaidi katika nchi za eneo la magharibi na Sahel barani Afrika. Kundi la Boko Haram ni moja ya makundi ya kigaidi ambayo yameimarisha harakati zao za kuteka nyara wanafunzi huko Nigeria. Mbali na kuua makumi ya raia wasio na hatia, kundi hilo limekuwa likiteka nyara wanafunzi wa shule wakiwemo wasichana na wavulana, kama tilivyoshuhudia katika miezi ya karibuni ambapo magaidi walishambulioa shule moja katika jimbo la Katsina, kaskazini mwa Nigeria na kuteka nyara wanafunzi 300. Hivi sasa kundi hilo limeteka nyara tena wavulana wengine 300.

Boko Haram inaharamisha masomo kwa wanafunzi, na hilo lilithibitishwa wazi na kiongozi wa kundi hilo aliyetoa ujumbe wa sauti akisema wazi kuwa lengo la kushamabuliwa shule moja ya bweni katika mkoa wa Katsina lilikuwa ni kupambana na masomo ya Kimagharibi. Hata kama serikali ya Abuja imekuwa ikifanya juhudi kubwa za kuachiliwa huru wanafunzi hao lakini hadi sasa haijafanikiwa katika hilo.

Kwa kuteka nyara wanafunzi, magaidi wa Boko Haram wanakusudia kuibua wahka na hofu miongoni mwa raia na wakati huo huo kuwatumia wanafunzi kama askari wao wa vita. Wengi wa wanafunzi waliotekwa nyara wamekuwa wakitumika katika shughuli za uagidi na kujilipua baada ya kupewa mafunzo maalumu ya kijeshi.

Makundi ya kigaidi yanaendesha shughuli zao za uagidi kwa madhara ya watu wa Nigeria katika hali ambayo Rais Muhammadu Buhari wa nchi hiyo katika kapmeni zake za uchaguzi aliahidi kuyatokomeza kabisa makundi hayo na kurejesha amani na usalama katika nchi hiyo. Licha ya kuwa amekuwa madarakani kwa muda mrefu sasa lakini hadi hajawasilisha mpango wowote wa muda mrefu wa kupambana na makundi hayo, bali ametosheka tu kwa kupiga nara zisizotekelezwa kivitendo.

Katika miaka ya karibuni serikali ya Nigeria imeimarisha uhusiano wake wa kisiasa na kiuchumi na nchi kama vile Saudia Arabia na ili kunufaika na utajiri wa nchi hizo, imekuwa ikitekeleza siasa ambazo zinalinda maslahi ya nchi hizo bila kujali iwapo zinadhuru maslahi ya raia wa nchi hiyo au la.

3956640

captcha