IQNA

Ndege za kivita zisizo na rubani za Yemen zalenga Saudia

13:04 - March 05, 2021
Habari ID: 3473704
TEHRAN (IQNA) – Ndege za kivita zisizo na rubani (drone) za Jeshi la Yemen zimelenga maeneo muhimu ya kijeshi na kibiashara nchini Saudi Arabia katika fremu ya oparesheni za ulipizaji kisasi.

Msemaji wa Majeshi Yemen Brigedia Jenerali Yahya Saree amesema majeshi ya Yemen yamelenga viwanja viwili muhimu vya ndege ndani ya Saudia.

Amesema katika hujuma ya mapema Ijumaa asubuhi, drone za kivita za Yemen zimeshambulia  maeneo muhimu ya uwanja wa ndege za kivita wa Mfalme Khalid na uwanja wa kimataifa wa ndege wa Abha.

Jana Alhamisi Brigedia Jenerali Yahya Saree alitangaza habari ya kufanyika shambulio jingine katika taasisi za mafuta za Saudi Arabia, ARAMCO.

Televisheni ya al Aalam ilimnukuu Saree akitangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, shambulizi hilo limefanyika kwa mafanikio katika eneo lililoainishwa kabla, la taasisi za mafuta za Saudia.

Yahya Saree amesema mashambulizi hayo ni katika kujibu jinai za utawala wa Saudia ambao unaongoza muungano wa kivita ulioanzisha vita dhidi ya Yemen.

3957643

Kishikizo: yemen saudia vita
captcha