IQNA

Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni washambulia Wapalestina Ukingo wa Magharibi, Msikiti wa Al Aqsa

16:49 - March 28, 2021
Habari ID: 3473766
TEHRAN (IQNA) – Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamewashambulia Wapalestina ambao walikuwa wakiandamana katika Ukingo wa Magharibi kupinga ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa taarifa, wanajeshi hao wa Israel wametumia risasi za plastiki na gesi ya kutoa machozi kuwashambulia Wapalestina katika kijiji cha Kafr Qaddum na kuwajeruhi watu kadhaa akiwamo mvulana wa miaka 15.

Kwingineko wanajeshi wa Utawala wa Kizayuni wa Israel wameshambulia Waislamu waliokuwa katika Msikiti wa Al Aqsa kwa ajili ya Swala ya Ijumaa.

Katika miaka ya hivi karibuni, utawala wa Kizayuni wa Israel umeshadidisha hujuma na uvamizi wake dhidi ya maeneo ya Wapalestina ukifanya njama za kufikia malengo yake haramu katika ardhi za Wapalestina.

Msikiti wa al-Aqsa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu umekuwa ukiandamwa na njama mtawalia za utawala vamizi wa Israel, hatua ambazo zinakwenda sambamba na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina.

3474307

Kishikizo: israel palestina aqsa
captcha