IQNA

Morocco yatangaza sheria ya kutotoka nje usiku Mwezi wa Ramadhani

18:26 - April 09, 2021
Habari ID: 3473797
TEHRAN (IQNA)- Serikali ya Morocco imetangaza kuwa itatekeleza sheria ya kutotoka nje usiku katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa ya serikali, sheria hiyo ya kutotoka nje itatekelezwa katika siku zote za Mwezi wa Ramadhani kuanzia saa mbili usiku hadi saa 12 asubuhi.

Kwa mujibu wa makadirio ya mwezi mwandamo katika baadhi ya nchi za Kiarabu, mwezi wa Ramadhani unatazamiwa kuanza Aprili 14. Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Morocco imesema itatangaza siku ya kuanza Ramadhani baada ya mwezi kuonekana.

Aidha Morocco imesema itaendelea kutekeleza sheria kali za kuzuia maambukizi ya COVID-19 nchini humo na wananchi wametakiwa kufuata maagizo yote ya kiafya.

Uamuzi huo wa kafyu uliotangazwa na serikali ya Morocco una maana kuwa Waislamu nchini humo watalazimika kuswali Sala ya Tarawih majumbani mwao mwaka huu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Mwezi wa Ramadhani mwaka jana pia watu wa Morocco waliswali Tarawih majumbani kufuatia uamuzi wa serikali kufunga misikiti ili kuzuia kuenea COVID-19.

3474395

captcha