IQNA

Kiongozi wa Ansarullah asisitiza kuhusu kurejea katika utamaduni wa Qur’ani

18:38 - April 10, 2021
Habari ID: 3473800
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah Sayyid Abdul-Malik Badreddin al-Houthi amesema Waislamu duniani kote wanapaswa kurejea katika mafundisho ya Qur’ani Tukufu.

Akihutubu kwa njia ya televisheni kwa mnasaba wa kukaribia Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Sayyid Abdul-Malik Badreddin al-Houthi amesema Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni wakati wa kuzingatia zaidi Qur’ani Tukufu. Aidha amesema njia ya kuwaongoza wanaadamu kuelekea katika saada ni Qur’ani Tukufu.

Kiongozi wa Ansarullah pia amesema kurejea katika mafundisho ya Qur’ani Tukufu kutamaliza mizozo na mifarakano katika ulimwengu wa Kiislamu.

Mwezi Mtukufu wa Ramadhani unatazamiwa kuanza Aprili 14 wiki ijayo ambapo mwaka huu sasa na mwaka uliopita, mwezi huu umegubikwa na janga la COVID-19.

Kwa kuzingatia kuwa Waislamu wengi watakuwa majumbani kutokana na kuenea janga la COVID-19  huo utakuwa wakati muafaka wa kusoma Qur’ani Tukufu na kutafakari kuhusu mafundisho yake.

3963360

 

captcha