IQNA

Saudi Arabia inatafakari kuzuia Mahujaji wa kimataifa

15:39 - May 06, 2021
Habari ID: 3473881
TEHRAN (IQNA)- Saudi Arabia inatafakari kuwazuia Mahujaji kutoka nje ya ufalme huo kwa mwaka wa pili mfululizo kufuatia ongezeko la aina mpya ya virusi vya corona.

Duru zinadokeza kuwa kuna mpango wa kuhakikisha kuwa Hija yam waka huu itatekelezwa tu na raia wa Saudi Arabia na baadhi ya raia wa kigeni wanaoishi ndnai ya ufalme huo ambao wamepata chanjo ya COVID-19.

Shirika la Habari la Reuters limenukulu duru ndani ya ufamle wa Saudia zikidokeza kuwa  mazungumzo yanaendelea lakini uamuzi wa mwisho haujachukuliwa.

Kabla ya janga la COVID-19 Waislamu karibu 2.5 millioni walikuwa wakishiriki katika ibad aya Hija kwa katika miji ya Makka na Madina ambapo Saudia kwa ujumla ilikuwa inapata pato la dola bilioni 12 kwa mwaka kutokana na Hija na Umrah.  Ufalme wa Saudia ulikuwa umepenga kufikisha mahujaji hadi watu miliioni 5 kufikia mwaka 2020 na umrha milioni 30 hadi mwaka 2030.

Imearifiwa kuwa Saudia sasa imesitisha kwa muda mpango wa kuwapokea Mahujaji kutokea njya ya nchi na kwamba itaruhusi tu Wasaudi na raia wa kigeni wanaoishi nchini humo na waliopata chanjo ya COVID-19 au wale ambao hawajaambukizwa corona katika kipindi cha miezi sita iliyopita.

Kuna mpango mwingine pia wa kuwaruhusu Mahujajikutoka nje ya Saudia kwa sharti la kuwa wamepata chanjo ya COVID-19 lakini kumeibuka mjadala kuhusu ni chanjo zipi zinakubalika na pia kuna wasiwasi kuhusu aina mpya ya virusi vya corona.

Mwezi Februari, Saudi Arabia ilipiga marufuku watu kutoka nchi 20 ili kuzuia kusambaa aina mpya ya kirusi cha corona. Waliopigwa marufuku kuingia nchini humo ni watu ambao wanawasili wakitokea nchi jirani ya Umoja wa Falme za Kiarabu, Ujerumani, Marekani, Uingereza, Afrika Kusini, Ufaransa, Lebanon, India, Pakistan na Misri.

3474636

Kishikizo: Corona saudi arabia hija
captcha