IQNA

Ayatullah Sistani awataka wapenda uhuru duniani waunge mkono Wapalestina

12:39 - May 12, 2021
Habari ID: 3473902
TEHRAN (IQNA)- Marjaa mkuu wa Kishia nchini Iraq kwa mara nyingine tena ametangaza uungaji mkono wake kwa 'mapambano ya kishujaa ya taifa lenye heshima la Palestina' katika kukabiliana na Wazayuni maghasibu na kutoa wito kwa mataifa yote huru duniani kuwaunga mkono Wapalestina.

Taarifa ambayo imetolewa na Ofisi ya Ayatullah Sistani, imesema: "Utumiaji mabavu ambao umeshuhudiwa hivi karibuni katika  Msikiti wa Al Aqsa na maeneo mengine ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu bila shaka unaoneysha muqawama wa Wapalestina mkabala wa ukatili na unyama wa wavamizi na pia uvamizi huo unaoendelea ni ishara kuwa maghasibu hawako tayari kuondoka katika ardhi walizopora." Amemuomba Allah SWT awasaidia Wapalestina kwani ni kwa uwezo Wake tu ndio watapata ushindi.

Ayatullah Sistani pia katika mkutano wake na Papa Francis Kiongozi wa Kanisa Katoloki duniani aliyetembelea Iraq mwezi Machi alikumbusha kuhusu kadhia ya Palestina na kusema kadhia hiyo ni mfano wa wazi wa kudhulumiwa na kukandamizwa taifa.

Katika siku za karibuni utawala ghasibu wa Israel umezidisha hujuma na mashambulizi yake ya kinyama dhidi ya Wapalestina wa Quds inayokaliwa kwa mabavu.

3971050

Kishikizo: sistani iraq quds palestina
captcha