IQNA

Wabahrain wamuenzi mfunguwa aliyefariki gerezani kutokana na COVID-19

14:11 - June 10, 2021
Habari ID: 3473994
TEHRAN (IQNA) - Mamia ya Wabahrain wamejitokeza kuandamana katika mji mkuu Manama, kumkumbuka mfungwa wa kisiasa ambaye amefariki kutokana na COVID-19 akiwa katika gereza la kuogofya ya utawala wa kiimla wa Aal Khalifa.

Maandamano hayo yamefanyika katika eneo la al-Diah Jumatano ambapo waandamanao walikuwa wamebeba mabango yenye picha ya 'Shahidi Hussein Barakat".

Baraka alikuwa kijana mwanaharakati wa Kiislamu ambaye alikuwa anashirikilia katika gereza la kuogofya la Jau kusini mwa Manama. Alikuwa anashikiliwa kutokana na kuwa ni mpizani ya ufalme wa ukoo wa Aal Khalifa ambao unatawala Bahrain kiimla. Aidha alilengwa kutokana na kuwa ni Mwislamu wa madhehebu ya Shia.

Utawala wa kiimla wa Bahrain ambao unapata uungaji mkono wa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel unawashikilia idadi kubwa ya raia katika magereza ambapo wafungwa hao wanateswa na kunyimwa matibabu. Hadi sasa wafungwa wengi wamefariki baada ya kunyimwa matibabu wakiwa gerezani.

Tangu Februari mwaka 2011, wakati ulipoanza mwamko wa Kiisamu Asia Magharibi, Bahrain imekuwa uwanja wa maandamano ya amani ya wananchi wanaopinga utawala wa kifalme wa ukoo wa Aal Khalifa.

Wananchi hao wanataka kuwepo uhuru, utekelezwe uadilifu, ukomeshwe ubaguzi na kuundwa serikali itakayochaguliwa na wananchi wenyewe.

Hata hivyo kwa msaada wa wanajeshi wa Saudi Arabia na askari usalama wa Imarati waliotumwa nchini Bahrain kupitia mpango wa ulinzi wa Ngao ya Kisiwa, utawala wa Aal Khalifa unatumia mkono wa chuma kukabiliana na matakwa ya wananchi hao.

Kwa mujibu wa duru za haki za binadamu, Bahrain ina idadi kubwa zaidi ya wafungwa wa kisiasa kulinganisha na idadi ya watu katika nchi hiyo ndogo zaidi katika Ghuba ya Uajemi.

3474923

captcha