IQNA

Haram Takatifu ya Bibi Masoumah SA, mjini Qom

19:32 - June 14, 2021
Habari ID: 3474004
TEHRAN (IQNA)- Jumamosi tarehe Mosi Dhilqaada 1442 Hijria sawa na Juni 12 mwaka 2021 ilisadifiana na siku ya kukumbuka kuzaliwa Bibi Masoumah SA.

Miaka 1269 iliyopita, kwa mujibu wa baadhi ya mapokezi ya wanahistoria, alizaliwa Bibi Fatima Maasuma, binti yake Imam wa Saba wa Ushia,  Musa al-Kadhim AS ambaye ni miongoni mwa wajukuu watukufu wa Bwana Mtume SAW. Fatima Maasuma AS alikuwa hatibu hodari, mwalimu mahiri, zahidi na mcha-Mungu mkubwa. Alipatwa na maradhi alipokuwa njiani kuelekea Khorasan huko Kaskazini Mashariki mwa Iran kwa ajili ya kumtembelea kaka yake yaani Imam Ali bin Musa al Ridha AS na akafariki dunia katika mji mtakatifu wa Qum baada ya kukaa hapo kwa siku 17. Leo hii ziara la mtukufu huyo linatembelewa na mamilioni ya waumini kila mwaka kutoka pembe mbalimbali za dunia. Hizi hapa chini ni picha za Ziara au Haram Takatifu ya Bibi Masoumah SA.

 
 
captcha