IQNA

Waislamu wanaongezeka Australia, misikiti haitoshi

20:47 - July 07, 2021
Habari ID: 3474079
TEHRAN (IQNA)- Waislamu wanaendelea kuongezeka maeneo mbali mbali ya Australia huku kukiwa na uhaba wa misikiti katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo.

Kati ya maeneo ambayo yameshuhudia ongezeko kubwa la Waislamu ni jimbo la Tasmania.

Kwa mujibu wa  Jumuiya ya Waislamu Australia, idadi ya  Waislamu imeongezeka maradufu tokea sense ya mwaka 2016 ambayo ilionyesha kuna Waislamu 2,498 katika jimbo la Tasmania.

Kuna msikiti mmoja tu katika jimbo hilo ambao uko katika eneo la Hobart.

Baadhi ya Waislamu hulazimika kusali Sala ya Ijumaa katika chumba kimoja kidogo katika Chuo Kikuu cha Tasmania eneo la Newnham. Baadhi ya wanaosali hapa hulazimika kusafiri kutoka eneo lenye umbali wa kilomita 160 kwa muda wa msaa mawili ili kushiriki katika Sala ya Ijumaa katika chumba hicho ambacho sasa hakina nafasi tena kwa ajili ya Waislamu wanaozidi kuongezeka.

Dkt. Rabiul Islam, mhadhiri katika chuo hicho anasema jamii ya Kiislamu imeshuhudia mabadiliko makubwa katika kipindi cha miaka minane iliyopita.  “Nilipofika hapa mwaka 2013 tulikuwa familia 40 hadi 50 lakini sasa tuna familia 500 na hivyo nafasi hii haitoshi tena,” amesema.

Mjini  Launceston katika  jimbo hilo la Tasmania, Waislamu wanapanga kununua jengo ambalo litabadilishwa kuwa  msikiti katika eneo la King Meadows. Tayari mkakati wa kuchangisha fedha  unaendelea na inatazamiwa kuwa msikiti huo utafunguliwa kabla ya mwisho wa mwaka huu wa 2021.

Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2016, idadi ya Waislamu Australia ilikuwa ni 604,200 au asilimia 2.6 ya watu wote wa nchi hiyo, hilo likuw ani ongezeko la asilimia 15 ililinganishw ana miaka mitano kabla.

3475167

Kishikizo: australia waislamu
captcha