IQNA

Waislamu wachache washiriki ibada ya Hija mwaka huu kutokana na vizingiti vya Saudia

20:16 - July 18, 2021
Habari ID: 3474111
TEHRAN (IQNA)- Ibada tukufu ya Hija ilianza rasmi jana chini ya usimamizi na sheria kali za kukabiliana na maambukizo ya virusi vya Corona huku idadi ya Mahujaji ikiwa chache mno kutokana na vizingiti vilivyowekwa na utawala wa Saudia.

Wizara ya Hija ya Saudi Arabia imetangaza kuwa, jana Ibada ya Hija ilianza baada ya Mahujaji kuingia Makka na kufanya tawafu.

Baadaye leo Jumapili Mahujaji wa nyumba ya Mwenyezi Mungu wanatarajiwa kuelekea Arafa wakijitayarisha kwa ajili ya kisimamo cha Arafa ambapo siku ya Jumanne watakuwa wakiteketeza moja ya nguzo muhimu za Hija yaani kuchinja na kusherehekea sikukuu ya Idi al-Haj.

Duru mbalimbali zimeripoti kwamba, kama ilivyokuwa mwaka jana, mwaka huu pia idadi ya Mahujaji ni ndogo mno ikilinganishwa na miaka ya nyuma ambapo walioruhusiwa kuhiji mwaka huu ni raia 60,000 tu wa Saudia tena waliopiga chanjo ya corona.

Hata kama idadi ya mwaka huu ni kubwa ikilinganishwa na mwaka jana, lakini bado ni ndogo mno ikilinganishwa na Mahujaji waliokuwa wakifanya ibada ya Hija miaka ya nyuma kabla ya kuibuka balaa la corona.

Mwaka 2019 karibu Mahujaji milioni 2.5 walitejkeleza ibada ya Hija kutoka maeneo mbalimbali ya ulimwengu.

Uamuzi wa Saudi Arabia wa kupiga marufuku ibada ya Hija kwa Waislamu kutoka nje ya nchi kwa mwaka wa pili mfululizo, licha ya kwamba umetajwa kuwa umechukuliwa ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona, lakini kwa hakika, unaenda sambamba na malengo ya Marekini na Israel na si ajabu kwamba umebuniwa na kupikwa Washington na Tel Aviv.

/3475280

captcha