IQNA

Palestina yapongeza Klabu ya Soka ya FC Barcelona kukataa kucheza na klabu ya Israel

21:01 - July 18, 2021
Habari ID: 3474112
TEHRAN (IQNA) - Shirikisho la Soka la Palestina limekaribisha hatua ya FC Barcelona ya Uhispania kukataa kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Beitar ya utawala haramu wa Israeli katika mji wa Quds (Jerusalem) inayokaliwa kwa mabavu.

Mechi hiyo ilipangwa kufanyika Agosti 4 huko Quds lakini FC Barcelona imetupilia mbali mwaliko huo.

"Tunatoa shukrani zetu kwa kilabu ya FC Barcelona kwa kujali hisia za mamilioni ya mashabiki wake ulimwenguni ambao walishangazwa na wazo kwamba kilabu ambayo inathamini haki za binadamu itacheza na moja ya vilabu vyenye ubaguzi zaidi ulimwenguni , ” Chama cha Soka cha Palestina kimesema katika taarifa.

Jibril Rajoub, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya kundi la Fatah na mkuu wa Chama cha Soka cha Palestina, alielezea hatua ya FC Barcelona ni "dhihirisho la uaminifu la utambulisho wa kweli wa Barcelona na heshima yake kwa mamilioni ya mashabiki wake ulimwenguni."

Mmiliki wa kilabu hiyo ya Israel, Moshe Hogg, alisema FC Barcelona ilikataa kucheza huko Quds na kwa hivyo aliamua kusitisha mechi hiyo.

Wapalestina wanashutumu mashabiki wa kilabu cha Beitar kwa ubaguzi wa rangi kwani walisikika mara kadhaa wakiimba kaulimbiu za kibaguzi dhidi ya Waarabu na matukufu ya Kiislamu.

3475281

captcha