IQNA

Rais wa Iran atangaza hatua za kukabiliana na janga la COVID-19

17:47 - August 14, 2021
Habari ID: 3474190
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Kupambana na Corona kwamba tayari ameidhinisha kununua dozi milioni 30 za chanjo ya COVID-19.

Rais Sayyid Ebrahim Raisi amesisitiza katika kikao hicho kilichofanyika leo mjini Tehran kwamba, ili kuweza kudhibiti na kusitisha maambukizi ya corona kuna udharura wa kuwepo azma na mshikamano wa kitaifa na kuongeza kuwa, sekta na asasi zote za serikali na zisizo za serikali, wananchi na maafisa wa serikali, wote kwa pamoja wanapaswa kushirikiana kwa ajili ya kudhibiti mambukizi ya ugonjwa wa COVID-19.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, wananchi katika maeneo na nchi zote za dunia wanapaswa kutayarishwa kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya corona.

Amesisitiza kuwa hatua nyingine muhimu katika mapambano hayo ni kuharakisha operesheni ya kutoa chanjo. Amesema tayari ununuzi wa dozi milioni 30 za COVID-19 kutoka nje ya nchi umeidhishwa na kwamba wataalamu wanaamini kuwa, kuna udharura wa kudhaminiwa dozi nyingine milioni 60 za chanjo ya kukabiliana na virusi hivyo ili kuweza kudhibiti hali mbaya ya sasa hapa nchini. 

Vilevile amesisitiza udharura wa kufuata na kutekeleza protokali na maagizo ya afya yanayotolewa na vyombo husika.

Mapema leo Wizara ya Afya ya Iran ilitangaza kuwa watu 466 wameaga dunia katika masaa 24 yaliyopita hapa nchini kutokana na virusi vya COVID-19. Katika kipindi hicho pia Wairani elfu 29,700 wamepatwa na virusi vya COVID-19.

3990653

Kishikizo: iran COVID-19 raisi rais
captcha