IQNA

Mashirika zaidi ya 400 katika ‘Wiki ya Halal’ huko Taiwan

22:15 - September 18, 2021
Habari ID: 3474310
TEHRAN (IQNA) – ‘Wiki ya Halal’ imeandaliwa kwa mara ya kwanza huko Taiwan kwa lengo la kuarifisha bidhaa na huduma ambazo zimetayarishwa kwa kuzingatia mafundisho ya Kiislamu.

Baraza la Ustawi wa Biashara ya Kimataifa Taiwan (TAITRA) limeandaa ‘Wiki ya Halal’ kwa njia ya intaneti ambapo washiriki wameweza kufanya vikao na kuonyesha bidhaa zao.

Katika maonyesho  hayo, bidhaa 60 ‘Halal’ ambazo zimetengenezwa Taiwan zimeonyeshwa ambapo mashirika zaidi ya 400 yameweza kuonyeshwa bidhaa hizo. Washiriki walikuwa ni kutoka nchi kama vile Indonesia, Malaysia, Ufilipino, Umoja wa Falme za Kiarabu na nchi kadhaa za Afrika.

Mashirika zaidi ya 400 katika ‘Wiki ya Halal’ huko Taiwan

Waandalizi wa mjumuiko huo wamesema maeonyesho hayo yataendelea hadi mwisho wa mwezi wa Oktoba kwa njia ya intaneti kwa kubonyeza hapa.

3998259

Kishikizo: taiwan waislamu halal
captcha