Kwa mujibu wa taarifa, taasisi ya Wakfu wa Kiislamu Italia imenunua jengo la kituo hicho kwa Euro milioni moja. Jengo hilo ambalo liko karibu na karakana za Shirika la Magari la Fiat.
Taasisi ya Wakfu wa Kiislamu Italia imesema kituo hicho cha Kiislamu kitakuwa kinatoa mafunzo mbali mbali kwa lengo la kustawisha ufahamu wa utamaduni wa Kiislamu miongoni mwa Waislamu.
Tayari mji wa Turan una misikiti 15 na inakadiriwa kuwa kuna Waislamu 60,000 mjini humo ambapo karibu nusu yao ni kutoka Morocco.