IQNA

Wenyeji asili wa Canada

Papa aombe radhi kufuatia jinai za Kanisa Katoliki Canada

12:01 - September 25, 2021
Habari ID: 3474340
TEHRAN (IQNA)- Wenyeji asili wa Canada wanasisitiza kuwa Papa Francis Kiongozi wa Kanisa Katoliki anapaswa kuomba radhi kufuatia ugunduliwa makaburi ya mamia ya watoto wa Wacanada asili waliokuwa wakishikiliwa kwa lazima katika shule za wamishonari wa Kikatoliki nchini humo.

Wito huo umetolewa hata baada ya Kanisa Katoliki la Canada kutangaza Ijumaa kuwa linawaomba radhi wenyeji asili nchini humo kutokana na jinai zilizotenfwa katika shule zilizoansihwa na serikali na kusimamiwa na kanisa Katoliki.

“Sisi, Maasokofu wa Kikatoliki wa Canada tunabainisha masikitiko yetu na tunaomba radhi”, imesema taarifa ya Kanisa Katoliki.

Tangu mwezi Mei mwaka huu hadi sasa, kumegunduliwa maeneo manne yenye makaburi ya miili ya watoto hao wa shule za bweni za huko British Colombia, Saskatchewan na Manitoba. Mabaki ya miili ya watoto wasiopungua 1148 imepatikana katika kaburi la umati na makaburi mengine kadhaa yasiyo na majina ya watoto waliozikwa ndani yake. 

Ripoti ya Kamati ya Ukweli na Maridhiano ya mwaka 2015 imeonyesha kuwa, watoto wasiopungua 4,100 waliuliwa wakiwa katika shule za bweni za Wamishonari wa Kikatoliki au kutoweka. 

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani amesema kuwa, ripoti iliyotolewa inatia uchungu lakini bado hajaomba rasmi rasmi kwa niaba ya Kanisa Katoliki. 

3999932

captcha