IQNA

Mwakilishi wa Iran aibuka mshindi mashindano ya Qur’ani Croatia

21:28 - September 27, 2021
Habari ID: 3474350
TEHRAN (IQNA)- Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Sina Tabbakhi ameibuka mshindi katika Mashindano ya 27 ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur’ani Tukufu nchini Croatia.

Tabbakhi aliwasili Jumapili usiku katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Imam Khomeini na kulakiwa na maafisa wa ngazi za juu wa harakati za Qur’ani nchini.

Akizungumza na mwandishi wa IQNA, amesema alikuwa na furaha kubwa kushinda  taji hilo la kifahari. Amesema washindani wake wakuu katika mashindano hayo walikuwa ni kutoka Malaysia na Marekani ambao walichukua nafasi za pili na tatu kwa tarataibu.

Kuhusu mipango yake ya baadaye, amebaini kuwa analenga kushinda katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Aidha Tabbakhi anakusudia kuanzisha darsa za kuhifadhi Qur’ani kwa vijana.

Duru ya 27 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Croatia ilikuwa na washiriki kutoka nchi 18 zikiwemo Bosnia and Herzegovina, Turkey, Iran, Somalia, Serbia, Ufaransa, Norway, Malaysia, Qatar, Jordan, Marekani, Uhispania, Kuwait na Oman.

Jopo la majaji katika mashindano hayo lilijumuisha  wataalamu na wasomi wa Qur’ani kutoka Croatia, Ufaransa, Macedonia Kaskazini, Uturuki na Bosnia Herzegovina.

Mashindano hayo yameandaliwa na Jumuiya ya Masuala ya Waislamu Croatia kwa ushirikiano na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu Qatar, Jumuiya ya Kiislamu ya Zagreb na Sekretariati ya Mashindano ya Qur’ani Bara Ulaya.

4000559

captcha