IQNA

Siku tatu za maombolezo zatangazwa Lebanon, rais amuonya kinara wa wanamgambo

17:44 - October 15, 2021
Habari ID: 3474425
TEHRAN (IQNA)- Siku tatu za maombolezo zimetangaza nchini Lebanon baada ya watu saba kuuawa na wanamgambo wakati wa maandamano ya jana katika mji mkuu Beirut.

Naye rais wa Lebanon amebainisha masikitiko yake kutokana na mapigano na ufatulianaji risasi mjini Beirut huku akimuonya kiongozi wa kundi la wanagambo wa chama cha 'Vikosi vya Lebanon'.

Gazeti la Al Akhbar likiandika kuwa, punde baada ya ufyatulianaji risasi jana, Rais Michel Aoun wa Lebanon alimpigia simu Samir Geagea, kiongozi wa chama cha 'Vikosi vya Lebanon' na kumtahadharisha kushusu matukio hayo ya ufatulianaji risasi na kisha akamfahamisha bayana kuwa: 'Sitisha mchezo wako."

Gazeti hilo limeandika kuwa katika mazungumzo hayo, Geagea amedai kuwa wanamgmabo wake hawakuhusika katika mauaji ya jana  mjini Beirut.

Katika hotuba baada ya tukio hilo, Rais Aoun alilaani vikali ufyatulianaji risasi katika eneo la At-T'ayyunah.

Jana asubuhi makundi ya watu wa Lebanon wanaopinga utendaji kazi wa Tariq Bitar mkuu wa uchunguzi wa mlipuko wa Beirut waliandamana  mbele ya jengo la Idara ya Mahakama ambapo ghafla walifyatuliwa risasi na watu wenye silaha. Katika tukio hilo watu saba waliuawa shahidi na wengine zaidi ya sitini kujeruhiwa.

Kufuatia tukio hilo, Harakati za Hizbullah na Amal zimetoa taarifa na kuwataka wananchi wa Lebanon wawe watulivu na wasikubali kutumbukizwa katika 'fitina khabithi' na kutangaza kuwa, walishiriki katika kuwashambulia waandamanaji wanafungamana na chama cha 'Vikosi vya Lebanon."

4005066

Kishikizo: lebanon Beirut aoun geagea
captcha