IQNA

Upinzani waendelea kuhusu Israel kuwa mwanachama mwangalizi Umoja wa Afrika

20:47 - October 16, 2021
Habari ID: 3474431
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Algeria ameelezwa kusikitishwa kwake na hatua ya baadhi ya nchi ya kung'ang'ania utawala haramu wa Israel upatiwe hadhi ya mwanachama mwangalizi katika Umoja wa Afrika.

Ramtane Lamamra amesisitiza kuwa, inasikitisha kuona kuwa baadhi yya mataifa ya Kiafrika yameng'ang'ania msimamo wao wa kutaka Israel ipatiwe hadhi hiyo ya mwanachama mwangalizi katika Umoja wa Afrika (AU).

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Algeria ameeleza kuwa, suala hilo lililowasilishwa na Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat limejadiliwa kwa masaa kadhaa na Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Umoja wa Afrika lakini hakujafikiwa natija baada ya kuibuka mpasuko na mgawanyiko.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, suala hilo sasa linatarajiwa kujadiliwa katika mkutano ujao wa Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika  (AU) mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Uamuzi huo wa Moussa Faki unaendelea kupingwa vikali na nchi nyingi za Afrika na Kiarabu. Nchi nyingi zinaamini kuwa, kukubaliwa Israel kuwa mwanachama mwangalizi wa Umoja wa Afrika ni ukiukaji wa wazi wa  malengo ya ukombozi wa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Algeria na Afrika Kusini zinaongoza kundi la nchi zaidi ya 15 ambazo zinapinga Israel kuwa mwanachama mwangalizi wa Umoja wa  Afrika na imeonya kuwa, yamkini umoja huo ukasambaratika iwapo uamuzi huo hautabatilishwa.

2416424

captcha