IQNA

Misikiti Uholanzi inapekuliwa kinyume cha sheria

11:29 - October 17, 2021
Habari ID: 3474434
TEHRAN (IQNA)- Baadhi ya manispaa nchini Uholanzi zinafanya upekuzi na upelelezi wa siri kinyume cha sheria katika misikiti na taasisi za Kiislamu kupitia mashirika binafsi ya upelelezi.

Kwa mujibu wa gazeti la kila siku la NRC la Uholanzi, kwa uchache manispaaa 10 nchini humo zimekuwa zikifanya upelelezi wa siri kuhusu misikiti, maimamu, maafisa wa kamati za misikiti na wanaharakati Waislamu katika jamii. Kwa mujibu wa taarifa, manispaa ambazo zimehusishwa na upelekezi huo ulio kinyume cha sheria dhidi ya Waislamu ni pamoka na manispaa za Rotterdam, Delft, Almere, Huizen, Leidschendam-Voorburg, Zoetermeer, Veenendaal, na Ede. Gazeti hilo limeongeza kuwa, Manispaa ya Utrecht ilisitisha upelelezi huo baada ya kuibuka wasiwasi kuhusu faragha na mbinu zinazotumiwa.

Taarifa zinadokeza kuwa, taasisi moja inayojulikana kama NTA ambayo huishauri serikali kuhusu misimamo mikali ya kidini imepokea fedha kutoka idara ya kitaifa ya kuratibu usalama na kukabiliana na ugaidi ili kufanya upelelezi huo. Hadi sasa Euro laki tatu zimetumika katika mradi huo wa siri na kwamba wapalelezi walijiarifisha kama Waislamu au wageni na walikutana na watu kadhaa bila kubainisha utmabulisho wao asili.

Ripoti hiyo inasema serikali ya Uholanzi ilianzisha upelelezi huo kutokana na nafasi ya kundi la kigaidi la ISIS au Daesh katika vita vya Syria na hofu kuwa yamkini kundi hili limejipenyeza katika jamii za Waislamu nchini humo. Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu Uholanzi (SPIOR) inasema uchunguzi huo umeathiri vibaya imani waliokuwa nayo Waislamu kwa serikali ya nchi hiyo.

3476072

captcha