IQNA

Nujabaa: Askari wa Marekani watashambuliwa wakibakia Iraq baada ya 2021

11:35 - October 22, 2021
Habari ID: 3474456
TEHRAN (IQNA)- Msemaji wa Harakati wa Mapambano ya Kiislamu ya Al Nujabaa ya Iraq ametahadharisha kuwa wanajeshi wa Iraq watashambuliwa iwapo hawataondoka Iraq ifikapo mwisho wa mwaka huu wa 2021.

Msemaji wa Al Nujabaa, Nasr al Shammari ameyasema hayo katika mahojiano na Televisheni ya Al Sumaria.

Baada ya shambulio la kigaidi lililofanywa Januari 7,2020 na jeshi la Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad nchini Iraq la kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassem Suleimani, aliyekuwa kamanda wa kikosi cha quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na Abu Mahdi al Muhandis, aliyekuwa Naibu Mkuu wa jeshi la kujitolea la wananchi wa Iraq al Hashdu-Sha'abi pamoja na wenzao kadhaa walioandamana nao, bunge la Iraq lilipasisha mpango wa kutaka askari vamizi wa Marekani waondoke katika ardhi ya nchi hiyo.

Hata hivyo licha ya kupita zaidi ya mwaka mmoja tangu kupitishwa mpango huo, Marekani haijaheshimu agizo hilo la bunge na takwa la wananchi wa Iraq na hadi sasa inatoa kila aina ya visingizio ili iendelee kubaki kijeshi nchini humo.

Kwingineko katika mahojiano yake, Al Shammari amesisitiza kuwa, harakati ya Al Nujabahaitaki kujiingiza katika mashindano ya kisiasa na kwamba ni haki ya Wairaqi kuandamana kulaani untendaji dhaifu wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Iraq.

Amesema Harakati ya Al Nujabaa haiungi mkono chama chochoe cha kisiasa lakini imeorodhesha ukiukwaji uliofanya na tume hiyo wakati wa uchaguzi.

/3476141

captcha