IQNA

Jamhuri ya Azerbaijan yafunga tovuti ya IQNA

13:18 - October 26, 2021
Habari ID: 3474473
TEHRAN (IQNA) – Jamhuri ya Azerbaijan imewafungia watumizi wa inteneti nchini humo tovuti ya Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa.

Kwa mujibu wa taarifa utawala wa Baku imezuia upatikanaji wa tovuti kadhaa za kidini na pia tovuti kadhaa za mashirika ya habari ya Iran zenye maudhui za kidini kwa lugha ramsi ya nchi hiyo ambayo Azeri.

Watumizi wa IQNA katika Jamhuri ya Azerbaijan wanasema wameshindwa kufungua tovuti ya IQNA nchini humo. Kwa sasa IQNA inasambaza habari kwa lugha 21 ikiwemo lugha ya Kiazeri.

Hatua hiyo ya utawala wa Jamhuri ya Azerbaijan inakuja wakati ambao IQNA aghalabu huchapisha habari zinazohusiana na Qur'ani Tukufu na baadhi ya matukio muhimu ya kimataifa pasina kuingia mambo ya ndani ya nchi zingine.

Kwa muda mrefu IQNA imekuwa moja kati ya tovuti za kidini zenye wasomaji wengi katika Jamhuri ya Azerbaijan.

4007921

captcha