IQNA

Wairani waadhimisha siku ya kupambana na ubeberu wa kimataifa

18:26 - November 05, 2021
Habari ID: 3474517
TEHRAN (IQNA)- Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limetoa taarifa na kusema kuwa, Aban 13 (Novemba 4) ambayo ni siku ya kupambana na ubeberu nchini Iran, bila ya shaka yoyote imebadilisha kabisa mlingano wa nguvu kieneo na kimataifa.

Sehemu moja ya taarifa hiyo imesema kuwa, Aban 13 ina kumbukumbu ya matuko mengi makubwa katika historia ya Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran.

Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limetilia mkazo wajibu wa kulindwa na kuenziwa kumbukumbu za mashahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, kuendelea kuenzi nafasi tukufu ya mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu, Imam Khomeini MA na kusema kuwa, jeshi hilo liko imara na tayari wakati wote kulinda mipaka ya taifa hili na kupambana na maadui wa Mapinduzi ya Kiislamu chini ya uamirijeshi uliojaa busara wa Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.

Alkhamisi ya tarehe 4 Noemba 2021 imesadifiana na maadhimisho ya Aban 13 kwa kalenda ya Kiirani ambayo ni siku ya kupambana na ubeberu wa dunia humu nchini.

Miaka 42 iliyopita, yaani tarehe 13 Aban 1358 Hijria Shamsia iliyosadifiana na tarehe 4 Novemba 1979, wanafunzi wa chuo kikuu wa Iran walilivamia pango la kijasusi la Marekani mjini Tehran lililokuwa na ubalozi wa dola hilo la kibeberu baada ya kuongezeka njama za Marekani za kutaka kufanya mapinduzi mengine nchini Iran.

Kuna matukio mengine matatu muhimu sana katika historia ya Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran nayo yalitokea kwenye vipindi nyeti na muhimu sana katika tarehe hiyo hiyo ya Aban 13. Maadhimisho ya siku hiyo hufanyika kila mwaka kote nchini Iran.

4010552

Kishikizo: iran 13 aban
captcha